Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya majlisi ya kuomboleza misiba ya Ahlulbait (a.s).
Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Ataba tukufu, watumishi wake na kundi kubwa la zuwaru.
Mhadhiri wa majlisi Shekhe Abdullahi Dujaili ameongea mambo mengi, ameeleza historia ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na nafasi yao katika kufundisha Dini ya kiislamu.
Majlisi hiyo ni sehemu ya harakati za Ataba tukufu za kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) na kujikumbusha misimamo na kujitolea kwao katika Dini na ubinaadamu.










