Kitengo cha habari na utamaduni kimetoa muhadhara kuhusu nafasi ya mtu mwenye athari katika jamii kwa ugeni wa vijana kutoka Baghdad

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa muhadhara wenye anuani isemayo (Mtu mwenye athari) kwa vijana kutoka Baghdad.

Mkufunzi Sayyid Yusufu Yasiri amesema “Kituo cha Multaqal-Qamaru chini ya kitengo, kimetoa muhadhara kwa vijana kutoka Baghdad, ameongea kuhusu mtu mwenye athari na nafasi yake katika jamii, hususana katika sekta ya uongozi na athari ya kujenga kizazi chenye kujitambua”.

Akaongeza kuwa “Muhadhara umepata muitikio mkubwa, umejikita katika kueleza namna ya kuendeleza vipaji na kuimarisha utamaduni”.

Akabainisha kuwa “Kituo hupokea makundi ya vijana na kutoa mihadhara inayolenga kuimarisha uelewa wao, jambo hilo ni sehemu ya harakati inayofanywa kwenye mikoa tofauti”.

Wageni wameshukuru Atabatu Abbasiyya kwa kuwakaribisha na kuwaandalia ratiba nzuri iliyowaimarisha katika sekta ya utamaduni na maarifa ya Dini yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: