Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya mahafali ya wahitimu wapya wa semina za Ahkamu-Tajwidi zilizofanywa katika wilaya ya Hamza mashariki ya mkoa wa Diwaniyya.
Kiongozi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika wilaya ya Hamza chini ya Majmaa, Sayyid Bahaau Tamimi amesema: “Tumefanya mahafali ya wahitimu kumi na tano wa semina ya Ahkamu-Tajwidi, baada ya kuhudhuria semina hiyo kwa muda wa miezi minne, kwa ushiriki wa mihadhara miwili kila wiki”.
Akaongeza kuwa “Semina ilikuwa na awamu mbili, awamu ya kwanza wamefundishwa masomo ya awali na awamu ya pili wakafundishwa masomo ya juu na mbinu mbalimbali za usomaji wa Qur’ani tukufu”.








