Kamati ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya imefanya kikao cha kujadili namna ya kuongeza juhudi ya kukusanya misaada kwa ajili ya watu wa Iran na Lebanon.
Juhudi hiyo ni sehemu ya kutekeleza maelekezo ya Marjaa-Dini mkuu aliye himiza kusaidia watu wa Iran na Lebanon walio athirika kwa vita.
Wajumbe wa kikao wamekubaliana kuendelea kuchangisha misaada ya kibinaadam na kuweka mikakati endelevu ya utekelezaji, itakayosaidia kufikia idadi kubwa zaidi ya waathirika wa vita.
Atabatu Abbasiyya imeshatuma msafara wa misaada wa kwanza Iran, uliokuwa na tani 690 za bidhaa za chakula na vifaa-tiba.
Amma nchini Lebanon jiko lake linatoa huduma ya chakula kwa watu 5000 kila siku kwenye vitongoji tofauti.













