Kitengo cha ukanda wa kijani kibichi chini ya Atabatu Abbasiyya kimesema kuwa, viunga vyake vinaingiza karibu tani 35 za mazao sokoni kila mwezi.
Kiongozi wa idara ya kilimo Sayyid Tanwiri Swadiq amesema “Watumishi wa idara wanavuna mazao ya kilimo kila siku katika viunga vya ukanda wa kijani kibichi, kutokana na kuzingatia ulimaji wa kisasa, unaotumia mbolea zenye ubora mkubwa zinazolonda udongo na usalama wa mazao”.
Akaongeza kuwa “Kitengo kinavuna tani 35 za mazao mbalimbali kila mwezi, miongoni mwa mazao ni bilinganya, pilipili, tango, maharage na bamia, eneo linalolimwa linaukubwa wa mita za mraba elfu 9 ndani ya (Green House).
Akabainisha kuwa “Kilimo hicho kinalenga kulisha masoko ya ndani na kuimarisha sekta ya kilimo, ili kupunguza utegemezi wa kuagiza mazao ya kulimo kutoka nje ya nchi na kumpatia mwananchi mazao bora na salama”.









