Kitengo cha mahusiano kimefanya muhadhara kwa wanafunzi wa sekula kuhusu akili-unde

Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya muhadhara kuhusu akili-unde na mahusiano yake katika elimu, kwa wageni wa kisekula kutoka mji mkuu wa Baghdad.

Muhadhara huo ni sehemu ya ratiba ya kitamaduni iliyoandaliwa na kitengo kwa wageni, ilihusisha pia kutembelea malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) sambamba na kuangalia baadhi ya miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mtoaji wa muhadhara Sayyid Ali Fadhili amesema: “Muhadhara umehusu mada mbalimbali, umuhimu wa akili-unde, uhusiano wake katika kutengeneza habari na falsafa yake katika sekta hiyo”.

Akaongeza kuwa “Muhadhara ulikuwa unakamilisha program iliyodumu kwa siku tatu”, akabainisha kuwa ilikuwa ya pekee kwa kuhudhuriwa na walimu bobezi wa sekta ya habari, jambo lililochangia kuimarika mada na maudhui zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: