Kitengo cha utumishi kimesafisha maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya kimesafisha eneo linalozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Jambo hilo ni sehemu ya jukumu lake endelevu la kudumisha usafi katika njia zote zinazoelekea haram tukufu.

Kazi hiyo imehusisha kusafisha njia kuu na milango kwa kutumia vifaa maalum, kuondoa taka zinazoachwa na zuwaru, kuongoza matembezi yao na kuweka mazingira bora ya utekelezaji wa ibada ya ziara.

Jambo hilo ni sehemu ya ratiba ya kudumu inayotekelezwa na kitengo, kwa lengo la kudumisha usafi katika maeneo yote yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu, ili kuweka mazingira safi kwa ajili ya watu wanaokuja kufanya ziara katika mji mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: