Kituo cha utamaduni wa familia chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, kwa kushirikiana na idara ya afya ya Karbala, kimefanya program ya kitamaduni yenye anuani isemayo (Mwangaza na ubunifu) kwa watumishi wakike wanaofanya kazi kwenye taasisi ya afya ya mkoa.
Kiongozi wa idara ya harakati na mafunzo katika kituo, Bibi Ikhlasi Jawaad Kaadhim amesema “Program inahusisha muhadhara wa kitaalamu kutoka kwa Adhraa Ahmadi wenye anuani isemayo (Misingi ya utulivu wa familia), ameeleza mambo makuu yanayosaidia kujenga familia yenye mshikamano na uwezo wa kupambana na changamoto za kijamii”.
Akaongeza kuwa “Muhadhara umepata muitikio mkubwa kutoka kwa washiriki, amejibu maswali na kuelekeza namna ya kutatua migogoro ya familia”.
Program hiyo ni sehemu ya harakati za kituo zinazofanywa kwa kushirikiana na taasisi za serikali, kwa lengo la kumsaidia mwanamke na kuboresha kipaji chake, jambo ambalo huleta matokeo mazuri katika familia na jamii.






