Kitengo cha habari na utamaduni tawi la wanawake kimefanya kongamano la taasisi za kaskazini ya mji wa Dhiqaar

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya kongamano la kwanza kwa taasisi za kitamaduni kaskazini ya mkoa wa Dhiqaar mwaka huu wa 2026m.

Kongamano limeratibiwa na kituo cha Multaqal-Qamaru chini ya kauli mbiu isemayo (Kutoka katika chemchem ya Imamu Jafari –a.s- unapatikana utambulisho na uelewa wa utamaduni).

Mkuu wa kituo cha shekhe Haarith Dahi amesema “Kongamano limefanywa katika wilaya ya Shurtwa mkoani Dhiqaar, kwa ushiriki wa zaidi ya taasisi 20 za kitamaduni kutoka vitongoji tofauti”.

Akaongeza kuwa “Kongamano limepambwa na ujumbe wa ufunguzi na michango ya wawakilishi wa taasisi washiriki, ikafuatia nadwa ya kielimu kuhusu utambulisho na umuhimu wake, sambamba na kuangazia nafasi ya taasisi za kitamaduni kwa vijana”. Akasema: “Kongamano limepambwa na fikra kutoka katika turathi za Imamu Jafari Swadiq (a.s)”.

Akabainisha kuwa “Kongamano hili ni maalum kwa taasisi za mkoa wa Dhiqaar, linatarajiwa kupanuliwa zaidi katika miaka ijayo ili lihusishe sehemu kubwa na taasisi nyingi zaidi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: