Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imewapa zawadi wanafunzi wake walioshika nafasi za kwanza kwenye shindano la kuhifadhi Qur’ani tukufu katika mkoa wa Muthanna.
Hafla ya utoaji wa zawadi imeandaliwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Muthanna chini ya Majmaa.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyosomwa na Hussein Ali Jubairi, ukafuata ujumbe wa mkuu wa Maahadi Shekhe Qudama Hadharami, amewapongeza wanafunzi na wazazi wao kwa mafanikio hayo makubwa, akasisitiza kuwa Maahadi itaendelea kulea vipaji hivyo.
Hafla ikahitimishwa kwa kugawa tuzo za midani na vyeti kwa wanafunzi walioshinda kwenye mashindano ya kuhifadhi Qur’ani, aidha shukrani za dhati zimetolewa kwa walimu na wazazi wao kutokana na juhudi kubwa walizofanya katika kuwalea na kuwafundisha vijana hao.






