Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya imefanya warsha yenye anuani isemayo (Mbinu za mhadhiri mwenye kuathiri na kukinaisha) katika jiji la Baghdad

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya Atabatu Abbasiyya, imefanya warsha yenye anuani isemayo (Mbinu za mhadhiri mwenye kuathiri na kukinaisha) katika mji mkuu wa Baghdad.

Kiongozi wa idara Shekhe Abduswahibu Twaiy amesema: Warsha imefanywa kwa kushirikiana na kituo cha masomo ya Qur’ani na qaswida za Husseiniyya katika mkoa wa Baghdad, ilikuwa na mada nyingi zinazohusu mbinu za kuathiri na njia za kukuza vipaji.

Akaongeza kuwa Atabatu Abbasiyya hufanya warsha hiyo kwenye mikoa tofauti ya Iraq, kutokana na umuhimu wake katika kukuza uwelewa wa jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: