Kitengo cha stoo chini ya Atabatu Abbasiyya kimeonyesha bidhaa mbalimbali kupitia idara ya mauzo, ikiwa ni sehemu ya utoaji huduma endelevu kwa zuwaru.
Kiongozi wa idara hiyo, Sayyid Qahtwani Jaasim amesema: Idara huandaa na kuuza bidhaa zinazohusiana na Ataba tukufu, jambo ambalo huwawezesha zuwaru kuzipata kwa urahisi.
Akaongeza kuwa, bidhaa zilizo inyeshwa zinajusisha miswala iliyotumika katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), viti vya kuswalia wazee (wasioweza kusimama), viti-mwendo vya watu wenye ulemavu na wenye mahitaji maalum pamoja na vyombo vya nyumbani.


