Idara ya wahadhiri tawi la wanawake imeanza kufanya semina za majira ya kiangazi zenye anuani isemayo vyanzo vya maarifa

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imeanza kufanya semina za majira ya kiangazi zenye anuani isemayo (Vyanzo vya maarifa).

Kiongozi wa idara bibi Taghrida Tamimi amesema: Semina zinazofanywa na Maahadi ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya idara, zinalenga wanafunzi wa sekondari na vyuo wanaopenda kujifunza mbinu za uhadhiri wa Husseiniyya, ikiwemo mahadhi na maqamaat, ikiwa ni pamoja na masomo ya Qur’ani na historia.

Akaongeza kuwa program inahusisha masomo ya habari, upigaji wa picha, kazi za mikono, kwa namna ambayo inasaidia kukuza uwezo wa washiriki kielimu.

Akabainisha kuwa idara hufanya semina hizi kila mwaka, kutokana na umuhimu wake katika kukuza vipaji vya uhadhiri wa Husseiniyya na kuimarisha uelewa wa Dini na utamaduni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: