Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimeadhimisha utukufu wa Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s) kufuatia kumbukizi ya kuzaliwa kwake.
Hayo yapo katika muhadhara uliotolewa ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kutoka kwa Shekhe Swalahu Karbalai mbele ya kundi la zuwaru.
Karbalai ameeleza historia ya Imamu Ridhwa (a.s) na nafasi yake kielimu, aidha amehimiza ulazima wa kuhuisha kumbukizi hizo na mafungamano yake na Ahlulbait (a.s).
Muhadhara huo ni sehemu ya harakati za kitengo cha Dini za kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) na kusambaza elimu yao na utukufu wao.


