Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imehuisha kumbukizi ya kuzaliwa Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s) kupitia kikao cha usomaji wa Qur’ani katika jiji la Baghdad.
Kikao cha usomaji wa Qur’ani tukufu katika mji wa Baghdad kimeandaliwa na Majmaa.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Ali Jawaad, ukafuata muhadhara kutoka kwa muwakilishi wa Marjaa-Dini mkuu Shekhe Abduljabaar Mahmadawi, ameeleza historia ya Imamu Ridhwa (a.s) na nafasi yake kielimu, ukafuata utenzi kutoka kwa Ali Dhahabi katika mazingira yaliyojaa furaha kutokana na maadhimisho hayo matukufu.
Hafla hiyo ni sehemu ya harakati zinazofanywa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika jiji la Baghdad, kwa lengo la kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s) na kujenga misingi ya kidini katika jamii.








