Wahudumu wa idara ya utumishi chini ya idara inayosimamia uwanja wa katikati ya Ataba mbili tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wamesafisha uwanja wa katikati ikiwa ni sehemu ya kazi zao za kila siku.
Kazi imehusisha kupiga deki na kusafisha maeneo hayo asubuhi, jioni na usiku, ili kuweka mazingira safi wakati wote kutokana na utukufu wa eneo hilo.
Jitihada hiyo ni sehemu ya mkakati unaolenga kutoa huduma bora kwa zuwaru na kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji wa ziara.




