Kitengo cha utengenezaji wa madirisha: Tumetengeneza herufi za kiislamu katika moja ya milango ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi matukufu na milango yake katika Atabatu Abbasiyya kimesema: tumetengeneza herufi za kiislamu katika moja ya milango ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa kitengo Sayyid Nadhim Ghurabi amesema: “Watumishi wa kitengo chetu wametengeneza herusi za kiislamu katika kiwanda cha Baabul-Muhsin (a.s), kwa lengo la kuuweka katika haram ya malalo takatifu, upande wa wanawake baina ya mlango wa kichwa kitakatifu na Hauraa Zainabu (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Kitengo kimeweka mkakati unaolenga kukarabati milango ya zamani, mafundi wameanza kukagua milango hiyo na kuifanyia ukarabati unaohitajika kwa kila mlango”.

Akaongeza kuwa “Kazi inaendelea katika mlango huo wenye urefu wa mita 2.58 na upana wa 1.97, miongoni mwa matengenezo ni kuweka madini ya fedha safi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: