Atabatu Abbasiyya imeweka vitu vya misaada katika vituo vya kusaidia wakimbizi nchini Lebanon

Atabatu Abbasiyya inaendelea kutoa misaada ta kibinaadamu kwa wakimbizi wa Lebanon, inagawa vitu mbalimbali vinavyo saidia kuboresha mazingira ya kuishi katika vituo vya wakimbizi.

Kiongozi wa kituo cha tafiti za kiislamu na kimkakati chini ya Ataba tukufu nchini Lebanon na mmoja wa wasimamizi wa ugawaji wa misaada, Shekhe Hassan Ahmadi Haadi amesema: “Msaada wa Atabatu Abbasiyya nchini Lebanon haujaishia kwenye jiko peke yake, bali inahusisha misaada mbalimbali wakati huu wa vita”.

Akaongeza kuwa: “Tumefanya kazi ya kuandaa vitu mbalimbali vya kusaidia, ikiwa ni pamoja na mashine za kufulia, mitungi ya gesi, usambazaji wa gesi na mahitaji mengine ya kila siku kwa familia za waathirika wa vita”.

Akaendelea kusema kuwa, miongoni mwa misaada inayotolewa kwa wakimbizi ni pesa taslim, maeneo yaliyofikiwa ni: Ghaziya, Nabtwiyya, Hubushi, Zahlah, Ba’alabaka, Harmal, mji wa Khurub na vijiji vinavyozunguka maeneo hayo, misaada yote inatolewa kwa kushirikiana na viongozi wa maeneo husika.

Jambo hilo ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa-Dini mkuu, aliyehimiza kusaidia watu wa Lebanon kutokana na athari ya vita inayoendelea, kwa kugawa mahitaji ya kibinaadamu kwa wakimbizi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: