Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, imefanya semina ya kuwajengea uwezo wasomaji wa mimbari ya Husseiniyya na wahadhiri.
Semina hiyo ni sehemu ya mkakati wa kuwajengea uwezo watumishi wa idara ya tablighi, kwa kuendeleza vipaji vyao na kuboresha uwezo wa kitablighi, ili kuwafanya waweze kutoa mihadhara bora na kupambana na fikra potofu.
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya kupitia semina hizi, inaimarisha nafasi ya mwanamke katika sekta ya tablighi, hususan kwenye mimbari ya Husseiniyya kwa kuandaa wahadhiri wenye uwezo wa kufikisha ujumbe wa dini kwa njia bora na yenye kuathiri katika jamii.



