Daru Uluum Nahajul-Balagha imetoa muhadhara wa kumi na mbili kwenye hafla ya kila wiki katika mkoa wa Dhiqaar

Daru Uluum Nahajul-Balagha katika Atabatu Abbasiyya, imetoa muhadhara wa kumi na mbili kwenye hafla ya Nahajul-Balagha inayofanywa kila wiku katika mkoa wa Dhiqaar.

Rais wa Daru Dokta Liwaa Atwiyya amesema kuwa: “Hafla hiyo ni sehemu ya harakati za Daru, inafafanua undani wa fikra za Nahaju-Balagha na kuileta karibu na jamii”. Akaongeza kuwa “Kikao kilikuwa maalum kwa ajili ya kuonyesha misingi ya malezi kutoka kwa kiongozi wa waumini (a.s)”.

Mtoaji wa muhadhara Shekhe Hani Rabii amesema, “Muhadhara umefafanua barua ya 28 miongoni mwa barua za kiongozi wa waumini (a.s)”, akabainisha kuwa “Imamu (a.s) alibadilisha upinzani kuwa nguvu na utukufu”.

Hafla hiyo ni sehemu ya jitihada za Ataba tukufu katika kuimarisha mafungamano ya watu na misingi ya maarifa inayo onyesha uwezo halisi wa mtu na jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: