Jarida la Riyadhu Zahraa (a.s) laendelea kupokea mada za mashindano yatakayo fanyika katika kongamano la wanahabari wakike

Maoni katika picha
Kufatia mambo yaliyo fanyika katika kongamano la wanahabari wakike la kwanza lililoendeshwa na jarida la Riyadhu Zahraa (a.s) lililo chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu yalitangazwa mashindano ya kielimu na ukafunguliwa mlango wa ushiriki katika mada zifatazo:

  • 1- Changamoto anazo kumbana nazo mwanahabari wa kike mwenye maadili.
  • 2- Namna ya kupambana na fikra potofu juu ya mwanahabari wa kike mwenye maadili.
  • 3- Fatwa ya wajibu kifai na nafasi ya mwanamke kuhusu fatwa hiyo husuusan mwanahabari wa kike.
  • 4- Nafafi ya wanahabari katika kumhami mwanamke na hatari za kijamii.
  • 5- Nafasi ya wanahabari katika kulinda historia isipotoshwe.

Mashindano haya yanalenga mambo yafatayo:

  • 1- Kuweka mkono katika matatizo ya wanahabari hasa wanayo kumbana nayo wanahabari wa kike wenye maadili.
  • 2- Namna ya kunufaika na uelewa wa wanahabari.
  • 3- Namna ya kujenga uhusiano bora wa wanahabari unaolinda heshima wa mwanahabari wa kike mwenye maadili mema.
  • 4- Namna ya kupambana na wanahabari wasiofaa.
  • 5- Umuhimu wa kusoma fani za majibu.
  • 6- Nafasi ya wanahabari katika kulinda historia.

Masharti ya mashindano ni:-

  • 1- Utafiti usiwe umesha wahi kuandikwa au kusambazwa na watu wengine (usikopi na kupesti).
  • 2- Utafiti uandikwe kwa kufata vigezo vya kielimu.
  • 3- Usiwe chini ya kurasa (10) za (A4) na zisizidi (15).
  • 4- Uandikwe muhtasari wa utafiti huo katika kurasa moja ya (A4) kwa hati ya (Arial) na saizi ya herufi iwe (14).
  • 5- Utafiti utumwe kwa CD au kupitia emeel ya jarida Riyadhu Zahraa, reyadalzahahra@alkafeel.net na mwisho wa kupokea ni 31/03/2017 m.
  • 6- Utafiti wowote ambao hautakua na sifa tajwa hapo juu hautazingatiwa.

Kutakua na zawadi zifatazo kwa tafiti zitakazo shinda:

  • 1- Mshindi wa kwanza: milioni moja dinari za Iraq.
  • 2- Mshindi wa pili: (750,000) dinari za Iraq.
  • 3- Mshindi wa tatu: (500,000) dinari za Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: