Maoni katika picha
Kiongozi wa idara ya wapiga picha na wahariri Ustadhi Bashiri Taajir aliiambia Kafeel kua:
“Kazi hii ni miongoni mwa mfululizo wa kazi za kitalamu tutakazo fanya, na tumemchagua huyu mtu mtukufu ambae ni fahari kwa historia ya uislamu na anaubora kwa waislam naye ni mzee Abuu Twalib (r.a) mu-umini wa makuraishi, kwa ajili ya kuangazia baadhi ya mambo katika uhai wa mwanajihadi wa kwanza katika uislamu na tuchangie katika kuondoa dhulma dhidi yake kutoka kwa wale wasiokua na elimu ya historia au wasio kua na insafu katika uhakiki na wengine ima kwa ujinga au kwa uadui dhidi ya Ahlulbait (a.s) au kutaka kuwanusuru maadui wa Ahlulbait (a.s) miongoni mwa bani Umayyah”.
Akaendelea kusema kua: “Filamu yenye muda wa dakika (27) imetokana na ubunifu wa Profesa wa Azhari bwana Khamisi Ahmadi ambae ni mtumishi wa idara hii, na imesha onyeshwa sehemu mbalimbali kama vile Iran, Lebanon, Sirya na sehemu zingine ambazo walipenda kuonyesha watoaji wa filamu hii, na walishiriki katika kuiandaa watalamu wa ndani na nche ya Iraq”.
Taajir aliendelea kubainisha kua: “Kutokana na vipengele vya filamu hii nilipata shauku ya kukutana na viongozi wa dini ndani na nche ya Iraq, na niliongea na viongozi hao katika kila kipengele cha filamu hii, miongoni mwa viongozi niliokutana nao ni, Shekh Ally Kurani, Ayatullahi Shekh Muhammad Sanad, Shekh Jafari Ibrahimiy vilevile mtafiti Sayyd Abdullahi Mussawiy na Sayyid Jafari Aamiliy hali kadhalika nilikutana na Mufti Ustadhi Othmani Rashadi na mtafiti wa kiislamu dokta Labibu Baidhun na nikakutana na Shekh Najmudini Twabasiy”.
Akaendelea kusema kua: “Mambo ya kihistoria yaliyo zingatiwa katika kazi hii yalitolewa ndani ya vitabu tegemezi vya hadithi na sira (vya kisunni na kishia) kisha yakawekwa katika kamati iliyo hakiki mambo ya kihistoria na usalama wa kifikra chini ya usimamizi wa Alama Shekh Ally Kurani na Sayyid Leeth Mussawiy rais wa kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na miongoni mwa vitabu vilivyo tumiwa ni, Biharul Anwaar, Swahihu Bukhari, Muniyatu Raaghibu fi imani Abuu Twalibi, Shaikhul batwiha-u, Mausuatul ghadeer, Bidaayatu wa nihaayah na Jawaahiru tareekh”.
Taajir alimalizia kwa kusema kua: “Filamu hii itaendelea kuonyeshwa katika mashindano ambayo Atabatu Abbasiyya tukufu itashiriki na katika maonyesho na makongamano ya kitaifa na kimataifa, kwa lengo la kueneza faida”.