Mfululizo wa hadhira za Qadiria: Kuhudhuria kwa ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika hafla ya maulidi ya mtume wetu mtukufu kumeonyesha nia njema na malengo bora, hakika ni mahudhurio mema na yameongeza furaha.

Maoni katika picha
Shekhe Khalidi Abdulqadir Alkilaniy ameonyesha furaha kubwa kwa kuhudhuria ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika hafla hiyo iliyo andaliwa na waislamu wa twariqa ya Qadiria kwa ajili ya kukumbuka kuzaliwa kwa mtume mtukufu, alisisitiza kua: “Hakika kuhudhuria kwa ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika hafla hii sambamba na ndugu zao wa madhehebu ya sunni kunaonyesha nia njema na malengo mazuri waliyo nayo, hakika kuhudhuria kwao ni jambo tukufu na kumeongeza furaha pia kunajenga umoja wa kitaifa kwa jamii zote za wairaqi”.

Akaendelea kusema kua: “Kitakacho tufurahisha zaidi ni kuendelea kukutana na kushirikiana katika minasaba hii na mingineo, na kupitia ugeni huu natuma salamu na shukrani zangu kwa wahusika wote wa Atabatu Abbasiyya tukufu vile vile natoa pongezi kwa waislamu wote kwa mnasaba wa kukumbuka kuzaliwa kwa mbora wa viumbe mtume wetu Muhammad (s.a.w.w)”.

Atabatu Abbasiyya tukufu ilituma ujumbe huo kwenda kushiriki katika hafla ambayo hufanyika kila mwaka kutokana na mualiko waliopata kutoka kwa jamii ya watu wa twarika ya Qadiria ambao hufanya hafla ya kukumbuka kuzaliwa kwa mtume mtukufu. Kushiriki kwetu kulipata muitikio mkubwa kwa kiasi ambacho kila aliye ongea alitoa ukaribisho rasmi kwa ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kushukuru kuhudhuria na kushiriki katika furaha hii pamoja na ndugu zao ahlusunna.

Wakibainisha kua, haya mahusiano na undugu chini ya bendera ya mtume wa uislamu Muhammad (s.a.w.w) yana msimamo na uwezo wa kusimama mbele ya maadui wa dini wanaofanya kila njia kuishambulia Iraq na raia wake vilevile ni mwanzo mzuri wa kujenga umoja wa waislamu na kuziunganisha jamii za wairaq wote hali kadhalika ni jibu kwa kufelisha njama za maadui wanaovuruga amani ya Iraq.

Hafla ilihudhuriwa na mashekhe wakubwa wote wakiwemo watafiti wa masomo ya akademik wa ndani na nje ya Bagdad, pamoja na mahudhurio makubwa ya wakazi wa Bagdad, ziliimbwa kaswida za kidini zilizo onyesha mapenzi kwa mtume Muhammad (s.a.w.w) na ziliburudisha masikio ya wahudhuriaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: