Kitengo cha malezi elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya chazungumza na Global house katika jiji la London kuhusu kufungua kituo cha kufundisha lugha ya kiingereza

Maoni katika picha
Baada ya mafanikio makubwa yaliyo fikiwa na kitengo cha kufundisha lugha ya kiengereza na kifarsi kwa wasio zielewa, tawi la kitivo cha masomo ya kibinadamu katika kitengo cha malezi na elimu ya juu, kutokana na malengo yake mazuri ya kupanua harakati hizi hadi kufikia kiwango cha elimu ya juu kwa wanafunzi wa kiiraq, kitengo hiki kimefanya mazungumzo na muwakilishi wa Global house katika jiji la London kwa ajili ya kufungua kituo kipya cha kufundisha lugha ya kiingereza.

Wakuu wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu ambao ni dokta Abbasi Mussawiy pia alikuwepo na msaidizi wa kitengo cha malezi dokta Mushtaqu Al-ally na msaidizi wa taaluma dokta Jasimu Ibrahimiy walifanya mazungumzo muhimu ya kujadili namna ya kushirikiana na kitengo cha kufundisha lugha ya kiingereza cha Uingereza (Global house) kwa kufungua kituo cha kufundisha lugha hiyo chini ya wataalamu wa kiengereza huku kikiongozwa na idara ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mwisho wa mazungumzo hayo, yalifikiwa makubaliano na dokta Yasini Answaariy muwakilishi wa Global house ya London na yakasainiwa makubaliano ya ushirikiano baina yao na kitengo cha kufundisha lugha katika chuo kikuu cha masomo ya kibinadam kitengo cha malezi na elimu ya juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: