Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chasonga mbele, kimekomboa kijiji cha Saadah na kugundua kiwanda cha kutengenezea vilipuzi na mabomu.

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinasonga mbele kufatia malengo yake kiliyo jiwekea, kutokana na wajibu waliopewa katika upande wa magharibi wa mji wa Mousol.. wamepata mafanikio makubwa yenye mashiko, wameweza kukomboa vijiji vingi vilivyo kua chini ya kikundi cha kigaidi cha Daish na kuwapa hasara ya nafsi na mali, na katika awamu hii ya sita wamefanikiwa kukomboa kijiji cha Saadah kilichopo kaskazini magharibi ya upande wa Tal abatwah magharibi ya mji wa Mousol.. kwa mujibu wa taarifa za kitengo cha matangazo cha kikosi.

Imeripotiwa kua: “Wakati wakiendelea na msako na upekuzi katika kijiji hicho waligundua kiwanda kilichokua kikitumiwa na magaidi katika kijiji hicho, kilikua na sehemu ya kutengenezea vilipuzi vya kurusha kwa mkono na vya kutega aridhini na sehemu ya kulainishia vyuma pia kulikua na sehemu ya kuunganisha na kufunga vyuma, vilevile kulikua na mahala pakutengenezea zana za kemikali za sumu zenye milipuko mikali, vitu vyote hivyo waliviacha baada ya kushindwa kwao vita mbele ya majemedari wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, na kikosi cha uhandisi kimesha rekebisha mazingira”.

Pia imeelezwa kwamba; Wapiganaji wa hashdi shaabiy wamefanikiwa kukomboa kijiji cha Khuwaitala magharibi ya mji wa (Ashwaah) paada ya mapambano na magaidi wa Daish, pia walifanikiwa kumuua gaidi wa kidaish aliyekua amevaa vilipuzi aliye taka kujilipua katika vikosi vilivyo kua vikielekea mji wa Ashwaah magharibi ya mji wa Tal afur, wapiganaji kutokea upande wa kusini wamekutana na wapikanaji kutokea upande wa kaskazini katika barabara inayo unganisha mji wa Tal abtwah na uwanja wa ndege wa (Shahid Sayyid Jaasim Aalishibri) na wamefanikiwa kuukomboa uwanja huo na vikosi vya wapiganaji wameanza kuutumia, na kufanikiwa kukata njia ya mwisho ya mawasiliano ya Daish na mji wa Tal afur katika upande wa kusini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: