Jioni ya leo (15 Rabiul Awwal 1438 h) sawa na (15 Desemba 2016 m) vilifanyika visomo viwili, chakwanza kilikua kisomo cha Qur an tukufu kilicho fanyika katika uwanja wa haram (sahani) ya Abuu Abdillahi Hussein (a.s) na cha pili katika uwanja wa haram (sahani) ya Abulfadhili Abbasi (a.s). visomo hivyo vilifanyika kama sehemu ya sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake imam Swadiq (a.s) ambazo hufanywa na Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) chini ya kauli mbiu isemayo: “Na hatukukutuma isipokua uwe ni rehema kwa walimwengu” na huendelea kwa muda wa siku tatu, walishiriki wasomi wa Qur an mashuhuri ambao ni: Mustwafa Alghalibiy, Rasulu Al amiliy, Adil Alkarbalaiy na Haidari Jalukhani. Waliburudisha masikio ya wahudhuriaji kwa aya za Qur an tukufu.
Washairi mahiri nao walisoma mashairi ya kuwasifu wenye mnasaba (mtume Muhammad s.a.w.w na imam Swadiq a.s) pamoja na ushujaa wa wapiganaji wa Hashdi Shaabiy, washairi walioshiriki ni: Ahmadi Zaamiliy, Saajid Almuhanna, Zainul-abideen Saidiy, Ally Hassan Alwan, Ahmad Alhujamiy na Hussam Alhamzawiy.