Sherehe ya maulidi ya mtume mtukufu na mjukuu wake imam Swadiq (a.s) yashuhudia vikao vya kitafiti katika siku yake ya pili

Maoni katika picha
Ratiba ya siku yapili katika sherehe ya maulidi ya mtume (s.a.w.w) na mjukuu wake imam Swadiq (a.s) inayo fanywa na Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) chini ya kauli mbiu ya: (Na wala hatukukutuma isipokua uwe ni rehema kwa walimwengu wote).

Ilifanywa majlisi ya kitafiti iliyokua na mihadhara miwili kuhusu uhai wa mtume wa rehema na mjukuu wake imam Swadiq (a.s) na namna alivyo julikana kwa elimu na fiqhi katika zama zake, hali kadhalika namna gani alikua anajibu maswali magumu, zikakumbushwa baadhi za riwaya zinazo thibitisha kwamba yeye ndie muanzilishi wa elimu ya kemia, pia ikaelezewa nafasi na hadhi kubwa aliyo kua nayo, kwa ushahidi wa riwaya nyingi kutoka katika vitabu vya pande mbili (sunni na shia).

Kisha ilizungumzwa mada ya pili na dokta Ally Hassanawiy mkuu wa kitivo cha masomo ya Qur an katika chuo kikuu cha Baabil, alizungumzia kua; Haiwezekani mtu aamini kua jukumu la kutafsiri Qur an na kuifanyika kazi liliisha baada ya kuondoka kwa mtume Muhammad (s.a.w.w), bali maimamu watakasifu waliendelea na jukumu hilo kwa ushahidi wa hadithi ya mtume (s.a.w.w) isemayo: “mimi nakuachieni vizito viwili kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumbani kwangu…” tukubali kua maimamu (a.s) walikua na elimu ya Qur an ya ndani kabisa.

Akabainisha kua; tunapo mzungumzia imam Swadiq (a.s) tunakuta kwamba alikua na upeo wa hali ya juu kabisa, naye ndiye madhehebu ya shia hunasibishwa kwa jina lake.

Baada ya kumaliza kutolewa kwa mada za kitafiti yalifanyika mashindano ya kuhifhadhi wasia wa imam Mahdi (a.f) kisha zikatolewa zawadi kwa walioshinda.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: