Kumalizika kwa sherehe za maulidi ya mtume (s.a.w.w) na mjukuu wake imam Swadiq (a.s) ambazo hufanywa kila mwaka.

Maoni katika picha
Ndani ya siku tatu mfululizo zimekua zikifanyika sherehe za maulidi kwa kushirikiana Ataba mbili tukufu (Husseiniya na Abbasiyya) na alasiri ya leo siku ya Juma Mosi (17 Rabiul Awwal 1438 h) sawa na (17 Desemba 2016 m) imefanyika hafla ya kufunga sherehe hizo katika ukumbi wa imam Hassan (a.s), sherehe hizi za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake imama Jafari (a.s) hufanywa kila mwaka na mwaka huu zilifanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Na hatukukutuma isipokua uwe ni rehema kwa walimwengu).

Hafla ilipata muitikio mkubwa na ilifunguliwa kwa Qur an tukufu iliyo samwa na msomaji mahiri Sayyid Haidari Jalukhani kisha ilifatia kaswida ya kimashairi iliyo somwa na dokta Karim Mudhhir Al amiriy iliyokua na anuani ya (Khadhwabun) mti umechipua.

Baada ya hapo kulikua na ushiriki wa Daru Rasulil Aadham (s.a.w.w) iliyo chini ya (Markazi Amid Duwaliy lilbuhuthu wa dirasaat) alipanda katika mimbari dokta Jawad Aali Nasrullahi akatoa mada kwa ufupi, iliyo kua na anuani isemayo: (Lulu ndani ya historia ya mtume mtakasifu).

Alizungumzia historia ya mtume mtukufu kuanzia kuzaliwa hadi kufariki kwake (s.a.w.w) na akataja riwaya nyingi zinazo elezea kila hatua ya umri wake, na hapo hapo alizikosoa baadhi za riwaya zilizo andikwa na wafalme kwa lengo la kushusha hadhi na heshima ya mtume (s.a.w.w) na wakajaribu kupambia baadhi ya hadithi, alisisitiza kwa waandishi wa historia kua wanatakiwa kuchukua historia ya mtume katika vitabu vinavyo aminika vikiongozwa na Qur an tukufu kisha hadithi za maimamu wa nyumba ya mtume (s.a.w.w).

Mada yake aliigawa katika sehemu zifatazo: kabla ya kuzaliwa kwa mtume, wakati wa kuzaliwa kwake, wakati ananyonya, kipindi cha kufariki mama yake (r.a) na kipindi cha kupewa rasmi utume na yaliyotokea baada ya kutangaza utume hadi kufariki kwake (s.a.w.w).

Baada yake yalifatia mashairi kutoka kwa mshairi mahiri Aqil Alhamdani, kisha kulitangazwa ufunguzi wa toghuti ambayo ni marejeo ya elimu, toghuti hiyo ni miongoni mwa miradi mikubwa iliyofanywa na kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, alisimama kiongozi wa toghuti hiyo ustadh Muhammad Abduswahibu na akatoa ufafanuzi kuhusu toghuti hiyo na vilivyomo miongoni mwa milango ya elimu katika Nyanja mbalimbali.

Hafla ilimalizika kwa kugawa makoja na vyeti kwa wale waliochangia kufanikisha kwa sherehe hii pamoja na waliofanikisha mradi wa tohgut ya marejeo ya kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: