Kitengo cha habari na utamaduni chazindua toghuti ambayo ni marejeo ya utafiti na elimu.

Maoni katika picha
Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu alasiri ya leo (17 Rabiul Awwal 1438 h) sawa na (17 Desemba 2016 m) kimezindua toghuti iliyo kusanya taarifa za kielimu na kitafiti, iliyo tengenezwa na idara ya masomo na utafiti (katika ofisi ya mambo ya kielektronik) kazi ya kuitengeneza imechukua karibu miaka mitatu, imeingizwa mada elfu sabini na program ishirini zilizo gawika sehemu tatu.

Habari hii imetangazwa katika hafla ya mwisho miongoni mwa hafla za kila mwaka za kusherehekea kuzaliwa kwa mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake imam Swadiq (a.s) ambazo hufanywa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya chini ya kauli mbiu: “Na wala hatukukutuma isipokua uwe ni rehema kwa walimwengu” na ilifanyika katika ukumbi wa imam Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya.

Mkuu wa idara ya mambo ya kieletronik ustadh Muhammad Abduswahibu Nasrawiy katika hutuba yake ya utambulisho wa mradi huu alisema kua: “toghuti (intanet) huchukuliwa kua ni maendeleo mapya katika ulimwengu wa kutafuta taarifa uzitakazo katika vyanzo muhimu na vinavyo kubalika, pia kuna mambo mengi ya kipekee, kama vile kupatikana kila kitu katika tafiti mbalimbali za kidini na kijamii”.

Akaendelea kusema kua: “uliwekwa muda wa kukamilisha mradi huu, tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumekamilisha katika muda uliopangwa, mradi ulianza kutekelezwa mwaka (2013 m) kazi imeendelea ya kuingiza mada hadi zimefika zaidi ya elfu (70) na inachukuliwa kua ni awamu ya kwanza ya mradi huu zitafatia awamu zingine, kama vile tarjama kwa ajili ya kufungua mawasiliano na tamaduni mbalimbali duniani na kuanzisha mtiririko wa machapisho ya kuonekana na kuyasambaza”.

Pia alifafanua kua: “hakika mambo muhimu yanayo tofautisha toghuti hii na zingine ni,

Kwanza: toghuti inaongozwa na wasomi waliobobea wa upande wa akademi na hauza.

Pili: toghuti inamtosheleza msomaji na kuperuzi toghuti zingine.

Tatu: toghuti inakiwango kikubwa cha mada.

Nne: vipengele vya toghuti vikuu na vidogo vinafika (1974).

Tano: mada zilizopo zimechukuliwa kutoka katika vyanzo muhimu.

Ikumbukwe kua; wazo la msingi katika mradi huu, nikuifanya iwe kichocheo cha utafiti kitakacho mnufaisha mwanafunzi wa masomo ya akademi na dini (hauza) na mada zilizo chaguliwa katika toghuti zinatokana na masomo na tafiti zilizo fanywa na wanazuoni wakubwa waliotoa katika vitabu muhimu vya kiislamu katika Nyanja mbalimbali za kielimu, ili uwe msingi unaokubalika katika kubainisha ukweli na kutoa elimu ya kidini na kijamii, ili kumsaidia mwanafunzi (mtu) anaye tafuta ukweli katika njia sahihi, hivyo toghuti inakua ni marejeo maalumu, jambo hili pekee linahitaji muda na juhudi kutoka kwa msomaji anapo amua kufanya utafiti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: