Idara ya wanawake kupitia jarida la Riyadhu Zahraa (a.s) ilihuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtume mtukufu na imam Jafari Swadiq (a.s) kwa kufanya nadwa yenye kauli mbiu isemayo: (Bibi Khadija baina ya jozi la mapenzi na kielelezo cha subira).
Tumeangazia mtu muhimu katika historia ya kiislamu ambaye ni bibi Twahiri Khadija (r.a), nadwa zinazo fanywa na jarida hili zitaendelea kuangazia mabibi watukufu katika nyumba ya mtume (s.a.w.w) ili kufahamu mazuri waliyo kua nayo na wao ndio vigezo vyema vya kuigwa na kufatwa, nadwa hizi zinafanyika katika ukumbi wa imam Hassan (a.s).
Nadwa hii imepata muitikio mkubwa kutoka kwa waheshimiwa wakina mama wasomi wa akademi na watafiti wa ndani na nje ya Ataba tukufu wakiwemo wakina mama waliowakilisha Ataba mbalimbali za hapa Iraq, na iliendeshwa kwa mtindo wa mahajiano kuhusu utukufu wa bibi Khadija bint Khuwailid (a.s) ambaye ujumbe wa mtume Muhammad (a.s) na mwanzo wa uislamu ulitegemea mali zake na upanga wa Imam Ali (a.s), vile vile katika nadwa hiyo lilishuhudiwa igizo la kuolewa kwa bibi Khadija na mtume Muhammad (s.a.w.w) hali kadhalika ilipambwa na visomo murua vya mashairi.
Ikumbukwe kua nadwa hii ni moja kati ya nadwa zinazo andaliwa na jarida Riyadhu Zahraa (a.s) lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuelezea utukufu wa wanawake wa nyumba ya mtume (s.a.w.w) kama vile, bibi Khadijatul Kubra, bibi Amina bint Wahbi, bibi Fatumatu Zzahraa, sayyidat Ummul Baneen (a.s) kisha zitaandaliwa historia zao tukufu na zitazungumzwa katika vikao vya nadwa.