Ushujaa wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wamaliza awamu ya kwanza ya jukumu lao magharibi ya Mousol na mkuu (mushrifu) wao asisitiza kubakia kwa wapiganaji katika mapambano..

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimemaliza awamu ya kwanza katika jukumu iliyopewa la kukumboa magharibi ya mji wa Mousol (wapiganaji maalum wa hashdi shaabiy) na chini ya kauli mbiu (Tunakuja ewe Nainawa) wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) wa Nyanja zote wamepambana vita kali na wameonyesha ushujaa wa hali ya juu.

Hayo yamezungumzwa katka taarifa iliyo tolewa na kikosi hicho, taarifa hiyo iliongeza kusema kwamba: “kikosi hiki kimeshiriki katika mapigano mengi yaliyo endeshwa na hashdi shaabiy katika awamu hii, na walikamilisha majukumu yote waliyo pewa na waliweza kukomboa kiasi cha kilometa (300) ikiwemo makumi ya miji na vijiji pia walitoa misada ya kibinadamu na kuzirejesha familia za wakimbizi majumbani mwao”.

Wakasisiza kua: “wabiganaji wa Nukhba na uingiliaji wa haraka wamebakia katika maeneo muhimu na wapo katika maandalizi kamili na wapo tayali kwa mapambano wakati wowote ikihitajika”.

Hali kadhalika mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji shekh Maitham Zaidiy amesema kua: “kimsingi tutabakiza wapiganaji katika uwanja wa mapambano na tuna andaa wapiganaji elfu tano watahadhari watakao kua tayali kuingia vitani wakati wowote ikihitajika hivyo”.

Ikumbukwe kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji vilishiriki vikosi vyake vyake mbalimbali katitika vita hii, vikiwemo kikosi cha deraya, vifaru, mabamu, kikosi cha Ummul Baneen (a.s), Alwiyatul kafeel, Alqamiy, Nnukhba, kikosi cha Maghaweer pamoja na vikosi vya anga (ndege), kikosi cha uangalizi wa kielektronik, kikosi cha upelelezi, na walifanya kazi kwa karibu zaidi na kikosi cha Imam Ali (a.s) kilicho chini ya Atabatu Alawiyya, na kikosi cha Answarul Marjiiyya na wapiganaji wa Muhammad Asgharu waliochini ya Mazuru (makumbusho) ya Sayyid Bakri bun Imam Ali (a.s) katika mji wa Baabil.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: