Chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Chuo cha teknolojia chafanya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtume Muhammad (s.a.w.w).

Maoni katika picha
Walimu na wanafunzi wa chuo cha teknolojia wamefanya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa wanadamu na mtume wa uislamu Muhammad (s.a.w.w) chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia mradi wa kijana wa kitaifa wa Alkafeel, kongamano la maulid lilikua na kauli mbiu isemayo: (kipenzi anayetarajiwa shifaa yake), ulihudhuria ugeni ulio wakilisha Ataba tukufu akiwemo muheshimiwa Shekh Hussein Aali Yasin muakilishi wa marjaa dini mkuu katika mji wa Kadhimiyya tukufu.

Hafla hiyo; iliyofanyika katika ukumbi wa chuo ilipambwa na mambo mengi, kwanza alizungumza Shekh Hussein Aali Yasin kisha akazungumza Sayyid Muhammad Mussawiy aliye toka katika Atabatu Abbasiyya tukufu halafu akazungumza Rais wa chuo hicho Dr. Amin Dawwai, wote walitoa pongezi kubwa kwa imam wa zama (a.f) na maraajii wa dini watukufu na umma wa kiislamu, mashariki na magharibi (dunia nzima) pia walitoa shukrani za pekee kwa wageni wa chuo waliohudhuria hafla hiyo ya kukumbuka mazazi ya mtume wetu mtukufu Abuu Qassim Muhammad (s.a.w.w), wakikumbusha ukamilifu na tabia njema ya hali ya juu kabisa aliyokua nayo mtume Muhammad (s.a.w.w) na namna alivyo simika mizizi yake, kutokana na ubora wa tabia yake uislamu ulienea katika kila kona ya dunia.

Hali kadhalika hafla ilipambwa na Qaswida zenye mashairi murua kuhusu mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s) na mwishoni ziligawiwa zawadi kwa walio fanikisha hafla hii.

Ikumbukwe kua Atabatu Abbasiyya tukufu huratibu na kusimamia kila mwaka makongamano mbalimbali ya kidini na kitamaduni kama sehemu ya harakati zake katika kulea jamii na kuiongezea uelewa wa dini na sehemu kubwa ya harakati hizi hufanywa katika vituo vya akademi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: