Kwa mwaka wa pili mfululizo chuo cha masomo ya kibinadamu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya kongamano kubwa la kusherehekea mazazi ya mtume chini ya kauli mbiu isemayo: (kwa mwenendo wake tumeongoka na tunaishi) kongamano hili linaingia katika mradi wa kijana wa kitaifa wa Alkafeel unao tekelezwa na idara ya mahusiano na vyuo vikuu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, lilifanyika asubuhi ya siku ya Juma Tatu (19 Rabiul Awwal 1438 h) sawa na (19 Desemba 2016 m) katika ukumbi wa Minasabati mikubwa ya chuo, kuna ugeni maalum ulio wakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu katika kongamano hilo ukiongozwa na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t).
Baada ya kisomo cha Qur an tukufu ya ufunguzi, ilisomwa surat Fat ha huku watu wakiwa wamesimama kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu wa Iraq, kisha ukaimbwa mwimbo wa taifa na mwimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu halafu katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya akaongea; alianza kwa kutoa pongezi kwa umma wa kiislamu na Maraajii dini watukufu kwa mnasaba huu kisha akasema kua: “Yatupasa kuzingatia mambo muhimu katika uzawa wa mtume Muhammad (s.a.w.w), uzawa mtukufu ulio watoa watu katika giza na kuwaingiza katika nuru kwani mtume ndiye nyumba ya elimu mbashiriaji na muonyaji aliye wahimiza watu kutafuta elimu na maarifa”.
Kisha Ashiqar alielezea mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika nyanja mbalimbali na hasa yakielimu kupitia shule za msingi za Ameed na chuo cha masomo ya kibinadamu, na miongoni mwa mafanikio waliyo fikia yanayo toa ushindani katika vyuo vya ndani na ncje ya Iraq, halikadhalika muheshimiwa katibu mkuu alizungumzia mafanikio katika mradi wa upanuzi wa upana na urefu wa chuo ambapo kutafunguliwa vitengo vipya na kuanzishwa kwa chuo kingine kitakacho itwa (chuo cha ameedul jaamia) katika mji wa Karbala mtukufu, kisha akawashukuru wakuu wa chuo kwa mafanikio ya aina yake waliyofikia katika nyanja ya kidini na kisekula kwa muda mfupi, hali kadhalika alisifu juhudi za walioandaa kongamano hilo na akawatikia taufiq.
Vilevile mkuu wa chuo Dr. Swafa-u Abduljabaar Ally Mussawiy alitoa khutuba iliyozungumzia sifa za mtume mtukufu (s.a.w.w) ili tuweze kufahamu taratibu za maisha yetu na tufate mwenendo wake mtukufu, pia alitoa shukrani za pekee kwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kufatia juhudi kubwa wanazo fanya za kukiendeleza chuo hicho ili kiwezo kutoa ushindani wa kielimu.
Pia kulikua na khutuba ya kisekula iliyotolewa na Shekh Swahib Naswaar iliyo zungumzia hadhi ya mtume Muhammad (s.a.w.w), pia kulikua na qaswida zenye mashairi mazuri ya kumsifu mtume Muhammad (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Kongamano lilimalizika kwa Atabatu Abbasiyya kutoa zawadi kwa wakuu wa chuo cha masomo ya kibinadamu zilizo kabidhiwa na mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu (d.b) halikadhalika walipewa zawadi wale waliofanikisha kongamano hili na wanafunzi walio faulu katika mashindano ya kitamaduni, baada ya hapo watu walielekea katika maonyesho ya vitabu na picha yanayo fanywa na Ataba mbalimbali pembezoni mwa kongamano hilo.