Kwa kuzingatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwalimu wa kwanza mtume Muhammad (s.a.w.w) na kutilia mkazo elimu hutolewa msaada kwa walimu na wanafunzi na kila anaye taka kujiendeleza kielimu katika hapa nchini.
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya mahusiano na vyuo, imetoa zawadi kwa walimu hodari wa chuo cha Jaamiatul Muthanna, nao ni wale walimu ambao majina yao yapo katika orodha ya walimu bora katika mwaka wa masomo (2015-2016 m) hii ni kwa ajili ya kuwatia moyo na kuwataka waongeze juhudi zaidi.
Hafla ya kutoa zawadi iliyo fanyika katika ukumbi wa chuo hicho ilipata mahudhurio makubwa kutoka kwa walimu na wanafunzi wao, wakiongozwa na rais wa chuo hicho Dr. Hassan Auda Alghanamiy na ugeni ulio wakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu. Hafla hiyo ilifunguliwa kwa kisomo cha Qur an tukufu kisha ulisomwa mwimbo wa taifa halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa hapa nchini.
Baada ya hapo ilisomwa khutuba ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo ilisomwa kwa niaba yake na shekh Dakhil Twaamah Annuriy kutoka katika kitengo cha mambo ya dini.
Alianza kwa kuwapongeza wahudhuriaji kwa kumbukumbu ya kuzaliwa mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wale imam Swadiq (a.s) akawafikishia salam na dua kutoka kwa kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbassiya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi. (d.i).
Kwa mahodari wa ufundishaji na wanafunzi wa chuo mfanyao kazi kwa juhudi katika kuitumikia Iraq na watu wake, kisha akasema: “Tunaishi katika siku tukufu za kukumbuka uzawa na mwalimu wetu wa kwanza aliye watoa binadamu katika giza na kuwaingiza katika nuru mtume wetu mtukufu Muhammad (s.a.w.w), yatupasa kufata nyayo zake na kufasiri kauli zake katika vitendo vitakavyo leta matokeo mazuri katika nyanja zote za maisha yetu na hasa katika nyanja ya kielimu”.
Kisha akaelezea nafasi ya imam Jafari Swadiq (a.s) katika nyanja ya elimu kwa kusema, “Alikua na chuo kikibwa kilicho toa wataalamu wakubwa waliobobea katika fani mbalimbali, na miongoni mwao ni Jaabir bun Hayyaani Alkuufiy, hakika imam huyu (Swadiq) ana hadhi kubwa sana pamoja na maimamu wote wa Ahlulbait (a.s), kutokana na umuhimu wa elimu, Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa umuhimu wa pekee kwa walimu na wanafunzi na hutoa mchango katika harakati mbalimbali za kielimu, na hizi zawadi ni sehemu ndogo katika swala hili”.
Akaendelea kusema kua: “Leo hii tumesimama mbele ya walimu wenye juhudi kubwa, walio jitolea muda wao kwa ajili ya kutoa huduma ya kimalezi na kielimu hadi wakawa ni miongoni mwa walimu bora na kuchaguliwa kupata zawadi ya Ataba tukufu, ambayo kwa hakika ni zawadi kutoka kwa Abulfadhili Abbasi (a.s), hongereni sana na Mwenyezi Mungu awawafikishe katika kuhudumia Nchi hii ambayo inakiu ya watu kama nyie”.
Kisha ilifatia khutuba ya rais wa chuo iliyo somwa na msaidizi wake wa kitengo cha taaluma ustadhi Qaasim Muhammad Halu, ambayo ilielezea namna anavyo thamini hatua hii ya Atabatu Abbasiyya tukufu kutoa zawadi kwa walimu bora wa chuo pia ikiwa ni miongoni mwa njia za kujenga mawasiliano na walimu wa sekula na kuwasaidia pamoja na kuwashajihisha kuongeza juhudi zaidi.
Kisha masikio yaliburudishwa kwa qaswida iliyo somwa na Dr. Abdulmutwalib Mahmudu ya kumsifu Abulfadhili Abbasi (a.s) na qaswida nyingine ikasomwa na mwanafunzi Maitham Aljaasimiy.
Halafu ikafatia khutuba kutoa kwa walimu walio pewa zawadi ambayo ilisomwa kwa niaba yao na Dr. Naajih Almayaaliy, ambapo alitoa shukrani za dhati kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa haya mazingatia yao mazuri, akasema: hakika hizi zawadi ni deni kwetu na amana katika shingo zetu inatakiwa tulipe kwa kuongeza juhudi zaidi kisha alimalizia kwa beti za mashairi murua ya kumsifu mtume Muhammad (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake watakasifu, na ikawa ndio mwisho wa hafla hii tukufu.