Kitengo cha turathi za Karbala kilicho chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimetenga muda wa kuangalia turathi za mkoa wa Karbala tukufu kwa kufanya nadwa na vikao kwa kitafikti.
Huzingatiwa nadwa na vikao vya kielimu kua moja ya njia zinazo tegemewa na kitengo cha turathi za Karbala kwa ajili ya kuangazia turathi muhimu zilizopo katika mkoa wa Karbala na miongoni mwake ni hii nadwa ya kitafiti iliyo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Turathi za Karbala katika jicho la wanasekula) na kwa anuani ya: (Turathi za Karbala katika utafiti wa kielimu) nadwa hii imefanywa kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Karbala kitivo cha malezi ya kielimu za kibinadamu.
Katika nadwa hii ziliwasilishwa tafiti 11 kutoka katika chuo cha Basra, Dhiqaar, Baabil na hapa Karbala, zote zilielezea turathi za Karbala, hususan kuhusu hauza na matukio yaliyo ikumba Karbala hali kadhalika msimamo wa watu wake katika baadhi ya matukio ya kisiasa na kijamii, vilevile msimamo wa wanazuoni wake katika matukio hayo pamoja na kuangazia matokeo (radi amali) ya misimamo yao kwa raia wa ndani na nje ya mkoa wa Karbala.
Nadwa ilikua na mahudhurio makubwa ya walimu na watafiti, pia kulikua na ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu ukiongozwa na katibu wake mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t), ambaye alikua na nafasi ya kuongea, katika mazungumzo yake alisisitizia umuhimu wa kuendelea nadwa hizi za kitafiti kwa ajili ya kudhihirisha yaliyofichikana katika turathi za mkoa huu, pia alitoa shukrani kwa chuo kikuu cha Karbala kwa ushirikiano wake na kitengo cha turathi za Karbala katika kufanya harakati hizi na uteuzi wa watafiti waliobobea katika historia”. Pia kulikua na khutuba ya rais wa chuo kikuu cha Karbala Dr. Munir Hameed Saadiy, alitoa shukrani kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuendesha na kusimamia makongamano ya kitafiti kama haya, na ukizingatia jambo hili ni moja ya mambo yanayo dumisha mawasiliano kati ya chuo na Atabatu Abbasiyya tukufu, sio katika hili jambo pekee kuna mambo mengi tunashirikiana katika kipindi cha mwaka mzima wa masomo.
Mkuu wa kitengo cha turathi za Karbala Dr. Ihsani Gharifi alitoa utambulisho wa kitengo na mambo wanayofanya pia alielezea mambo waliyo fanikisha kitaaluma na kitamaduni.
Pembezoni mwa nadwa hii yalifunguliwa maonyesho ya turathi yaliyo jumuisha idadi kubwa ya vitabu na majarida vilivyo chapishwa na vituo vya turathi vilivyo chini ya Ataba tukufu. Na mwisho wa nadwa viligawiwa vyeti vya ushiriki kwa watafiti na wasomi wa kisekula walio kuwepo, kwa ujumla walimu na wanafunzi wa vyuo wote walitoa pongezi kubwa kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na juhudi kubwa wanayo fanya katika vyuo vikuu ya kuzitambulisha turathi na umuhimu wake kwa kufanya nadwa kama hizi katika vyuo.
Ikumbuke kua lengo la makongamano haya ya kitafiti ni kuchangia katika kuwepo kwa maktaba na vituo vya kitamaduni na kielimu kwa ajili ya kufaya utafiti utakao angazia na kubainisha turathi za Karbala, hali kadhalika kuzileta pamoja juhudi za kisekula na kubadilishana uzoefu kati ya vyuo vikuu na walimu pamoja na vituo vya mambo ya turathi kwa ajili ya kuhuisha jambo hili.