Tawi la kitengo cha habari na utamaduni takika Atabatu Abbasiyya tukufu wakati wa ushiriki wao katika maonyesho ya Jaamiatu Aalulbait (a.s) yanayo fanyika nchini Iran katika mji wa Qum mtukufu wamepata daraja la kwanza katika mpangilio na vionjo vya maonyesho.
Kwa mujibu wa maelezo ya naibu rais wa kitengo cha habari na utamaduni Sayyid Aqeel Abdulhussein Alyaasiriy alipo ongea na Alkafeel alisema kua: “Hii heshima tuliyo pata sio bure, ni kwa sababu tumestahiki heshima hiyo kwa mujibu wa kamati ya maandalizi ya maonyesho, pia inatokana na uzowefu mkubwa walio nao watumishi wa kitengo hiki katika ushiriki wa maonyesho ya kitaifa na kimataifa, hivyo tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu ushindi kwao unakua ni jambo la wazi katika maonyesho mengi, na miongoni mwake ni katika maonyesho haya ambayo zimeshiriki taasisi za uchapaji na usambazaji nyingi za ndani ya Iran na nje, bado tawi letu limekua ni mahala ambapo anapana kila anayekuja kututembelea kile anacho kihitaji katika mambo ya kifikra na kiroho, kwa sababu limefungamana na jina la mbeba bendera ya imam Hussein (a.s), pia ushiriki huu huchukuliwa kua ni fursa ya kutambuana na taasisi za uchapaji na usambazaji za kimataifa”.
Akaendelea kusema kua: “Tawi letu lilipambika kwa machapisho mbalimbali ya kidini na kitamaduni yenye maudhui mbalimbali za kila umri, na jambo la pekee kwetu ni, machapisho yote yameandikwa na kuchapishwa na Ataba tukufu, hii ilikua sifa ya pekee ukilinganisha na taasisi zingine zilizo shiriki, vilevile eneo letu lilipambwa kwa picha za mnato za Atabatu Abbasiyya tukufu na miradi yake pamoja na huduma wanazotoa kwa mazuwaru”.
Ikumbukwe kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki mara nyingi maonyesho na makongamano ya kitaifa na kimataifa, inaendelea kupata muitikio mkubwa kutoka kwa watu na idadi ya machapisho yake huongezeka katika kila maonyesho hua ni tofauti na maonyesho yaliyo pita.