Matibabu bila malipo: Hospitali ya Alkafeel yaendesha mradi wa matibabu bila malipo katika miji na vijiji

Maoni katika picha
Pamoja na kufanikisha kwa miradi inayo endeshwa na hospitali ya rufani ya Alkafeel iliyopo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa mara nyingine wanafanya mradi wa matibabu bila malipo, kwa kuwatibu wakazi wa mjini na vijiji vilivyo karibu na mkoa wa Karbala pamoja na kuwafanyia vipimo na kuwapa dawa kulingana na majibu yao bure, kazi hii inafanywa na madaktari bingwa wa macho, tumbo na ngozi, hapo baadae tunatarajia kuongeza magonjwa mengine, na itakua kazi ya mzunguko wa muda na mahala kutokana na jeduali litakalo pangwa na idara ya hospitali.

Mradi huu unalenga yafatayo:

Kwanza: kutambua hali ya maradhi katika miji yenye upungufu wa vituo vya afya.

Pili: kufahamu tiba stahili na kutolewa tiba hiyo chini ya usimamizi wa daktari bingwa.

Tatu: kuchangia katika kupunguza matatizo ya kiafya kwa wakazi.

Nne: kuwazoesha wakazi wa miji hii kupima afya zao na kuwapa ushauri wa kidaktari.

Tano: kuondoa uzito wa kwenda hospitali na kusimamia matibabu yao stahili.

Sita: kufahamu kimaeneo maradhi yanayo wasumbua wakazi wa maeneo hayo na njia sahihi ya kuyatibu.

Ifahamike kua; mradi huu ulianzia katika mji wa Alwandi uliopo umbali wa kilometa (25) kutoka mjini Karbala, na tumewapina na kubaini matatizo zaidi ya (250) na wote tumewapa matibabu bure, mradi ulipata muitikio mzuri na mkubwa kwa wakazi wa mji huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: