Kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu abbasiyya tukufu ahudhuria hafla ya kumaliza daura ya Nurul Mubin katika Maahadi ya Qur an tukufu ya wanawake huko Najafu.

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur an tukufu ya wanawake katika mji wa Najafu iliyo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya juma Nne (20 Rabiul Awwal 1438 h) sawa na (20/12/2016 m) walifanya hafla ya kumaliza kwa wanafunzi wa awamu ya hamsini na tatu ya masomo hapo katika Maahadi, katika hafla hiyo alihudhuria kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu, Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) mahudhuria yaliumbika katika picha ya baba mtegemewa na mwalimu mlezi.

Sayyid Ahmadi Swafi alisisitiza umuhimu wa kuendelea kwa masomo katika Maahadi hiyo, hasa masomo ya Qur an tukufu, kutokana na faida kubwa inayo patikana katika jamii, pia alisifu mafanikio yaliyo fikiwa na Maahadi hiyo toka kuanzishwa kwake hadi leo, na akasisitiza umuhimu wa kumuiga bibi Fatumat Zahraa (a.s) kwani yeye ndio kiigizo chema kwa mwanamke wa kiislamu anaye taka kufata mwenendo wa Qur an.

Kisha ilifata awamu ya kugawa shahada na zawadi kwa wahitimu mbalimbali, ziligawiwa zawadi kwa wahitimu wa misingi sahihi ya ufundishaji wa Qur an, na wakapewa vyeti washiriki wa mashindano ya sura mbili (Yaasin na Rahmaan) pia walipewa shahada wahitimu wa masomo ya Ahkaami Tajweed, hali kadhalika wahitimu wa Ahbaab Kafeel awamu ya tatu, pia wakapewa zawadi wakina dada walio shiriki katika mradi wa vituo vya Qur an unao tekelezwa katika ziara za milionea (mamilioni wa watu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: