Katika mahala patakasifu uwanja wa haram ya Abulfadhili Abbasi (a.s) watumishi wa mradi wa vituo vya Qur an katika ziara ya arubaini wakirimiwa

Maoni katika picha
Alasiri ya leo Ijumaa (23 Rabiul Awwal 1438 h) sawa na (23 Desemba 2016 m) katika uwanja wa haram ya Abulfadhi Abbasi (a.s) imefanyika hafla ya kuwakirimu watumishi wa mradi wa vituo vya Qur an uliofanyika wakati wa ziara ya arubainiyya ya imam Hussein (a.s) na uliotekelezwa kwa mara ya kwanza. Kutokana na mafanikio makubwa yaliyo patikana, watumishi wa mradi huo wamepewa zawadi mbele ya kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) pia alikuwepo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) pamoja na wakirimiwa waliotoka katika mikoa tofauti.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur an tukufu, iliyosomwa na Sayyid Hussein Halu, kuandaa mazingira ya khutuba ya kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) ambaye baada ya salamu, alipongeza juhudi za watumishi wa mradi huu, alianza kwa kusema, “Huendha ni katika Baraka za imam Hussein (a.s) hakika ni nyingi mno Baraka zake, ni kukubaliana kwa watumishi kuwahudumia watu wanaokuja ziara ya arubaini kwa kupitia Qur an tukufu, limejitolea kundi la vijana walio muamini Mola wao kulipa umuhimu swala la Qur an, kundi hili lilijitokeza baada ya Ataba na Mazaru pamoja na baadhi ya taasisi za kitamaduni kuweka makusudio ya pamoja ya kuongeza umuhimu katika swala la Qur an tukufu ndipo juhudi hizi zikakusanyika chini ya kamati iliyo onyesha Dhahiri umuhimu wake juu ya Qur an”.

Akaendelea kusema kua: “Kamati hiyo kupitia taasisi za Qur an zilizo chini ya Ataba tukufu na Mazaru wamefanya juhudi kubwa, hakika tunasema wameweza kuwatoa vijana bora katika usomaji wa Qur an tukufu, hata tunaweza sema, nchi inajivunia uwezo mkubwa wa wasomaji hao wa Qur an tukufu”.

Kisha ilifatia khutuba ya uongozi wa juu unao onganisha kamati za Ataba na Mazaru matukufu, iliyo somwa na Sayyid Murtadhwa Jamaludini muwakilizi wa kamazi hiyo, naye alisema kua: “Bado Iraq inaendelea kutoa huduma zinazo staajabisha walimwengu, hakika ziara ya arubaini haikua kutembea kutoka baharini hadi mtoni, bali ni nchi na mabara yalitembea kumkirimu Hussein (a.s), na faida zilizo patikana kwa walimwengu kutokea Karbala tunatarajia Qur an pia ni miongoni mwake”. Akabainisha kua: “Kuna nafasi kubwa ya kunufaika na uongofu wa Imam Hussein (a.s) katika Qur an tukufu”.

Halafu ukafatia ujumbe wa muungano wa vikundi vya Qur an vya Iraq ulio somwa na katibu mkuu wa muungano huo Dr. Naatwiqu Zarkaani, alielezea huduma walizo toa kwa mazuwaru (watu walpiokuja kufanya ziara) na nafasi ya Qur an katika nhi hali kadhalika namna walivyo ratibu na kuendesha vituo vya Qur an katika ziara ya arubaini. Kisha hafla ilipambwa na mashairi ya kumsifu mtume yaliyo somwa na Sayyid Haani Almussawiy, halafu zikagawiwa zawadi kwa wahudumu wa mradi tajwa pamoja na vyeti vya ushiriki, kwa wale walioshiriki katika vituo vya Qur an vilivyo enea njia zote zinazo ingia Karbala tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: