Mapambo mapya yaupendezesha uwanja wa haram ya Abulfadhili Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Miongoni mwa hatua za mradi wa upanuzi wa haram tukufu, katika hatua ya uwekaji wa paa ya uwanja wa haram ya Abulfadhili Abbasi (a.s) ambayo ipo ukingoni mwa kukamilika ni kuwekwa mapambo katika paa hilo, nayo ni mapambo ya aina yake yenye ukubwa na vipimo maalumu yanao endana na mapambo yaliyopo, ili kuweka uwiano wa mapambo na nakshi zilizopo ndani na nje kwa upande mwingine.

Tumeagiza mapambo haya kutoka katika nchi ya Slovakia, inayo julikana kwa kutendeneza mapambo ya kifahari ya (Brillant crystal ligting) katika shirika lenye uzoefu wa zaidi ya miaka (50), tulitengenezesha mapambo haya rasmi kwa ajili ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na mahitaji ya uwanja wa haramu ya Abulfadhili Abbasi (a.s) pia kwa kufata ramani ya uwekaji wa mapambo haya ili yawezo kuoana kiuzito, nakshi na utumiaji wa umeme.

Ustadhi Ally Majhuul kiongozi wa idara ya mapambo katika kitengo cha ulezi wa haramu, alisema kua: “Idadi ya mapambo imefika (22) kila moja lina upana wa (mt, 3.2) na urefu wa (mt, 4.2) na lina taa (203) zilizo funikwa na myanvuli midogo midogo yenye umbo ya nusu duara iliyo chovya dhahabu na kutiwa nakshi ya kauli mbiu ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kutumia mikono”.

Akaendelea kusema kua: “Kila pambo lina matawi (105), tawi: ni kijifimbo kilicho chovya maji ya dhahabu ya Itali kisha kikawekwa karistali ili kupendezesha muonekano wake, hadi sasa hivi tumesha weka mapambo (6) manne upande wa kaskazini kuanzia mlango wa imam Ali Haadi (a.s) hadi katika mlango wa imam Mussa Kaadhim (a.s) na mapambo mawili upande wa magharibi, kuanzia mlango wa imam Swahibu Zamani (a.f) hadi katika mlango wa imam Hassan (a.s) tunatarajia katika siku chache zijazo kukamilisha nusu iliyo baki katika upande wa mashariki”.

Ifahamike kua kazi ya kuweka mapambo ina hatua mbili, hatua ya kwanza ni kuitengenezea njia maalumu ya umeme na hatua ya pili, kufunga vifaa vya mapambo ikiwepo matawi, mataa na viambatanishi vyake vyote, kazi ya kufunga pambo moja huchukua wiki nzima takriban.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: