Kitengo cha habari na utamaduni chaendesha semina na mawakili katika mkoa mtukufu wa Karbala.

Maoni katika picha
Kitengo cha habari na utamaduni idara ya fikra na ubunifu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya semina yenye maudhui isemayo (kuendesha mahojiano yenye tija na njia za kuathiri) kwa mawakili wa mkoa wa Karbala kwa kuwasiliana na chama cha mawakili tawi la Karbala.

Msimamizi wa semina ustadhi Sefu Bawi ambaye ni mtumishi wa ofisi ya uandaaji na uendelezaji katika idara ya fikra na ubunifu alifafanua kua: “Semina ilikua ni ya siku mbili, kila siku ilidumu kwa masaa nane, zilifundishwa mada zifatazo:

  • 1- Kufahamu malengo na aina za taratibu za mahojiano.
  • 2- Mbimu za kuendesha mahojiano yenye tija.
  • 3- Hatua za mahojiano.
  • 4- Vipi mahojiano yatafaulu.
  • 5- Sifa za mwenye kuhoji mwenye mafanikio.

Akaendelea kusemakua: “Ilipangwa semina hii kutokana na tabia iliyo zoeleka hapa Iraq pia kufatia maombi ya chama cha mawakili tawi la Karbala, hakika semina hii inalea vipaji na uwezo wa kufanya mahojiano yenye tija baina ya mtu na mtu, na jambo hili linahitajika zaidi na ndugu zetu mawakili kutokana na kazi yao”.

Aliye fanya mawasiliano ya kufanikisha semina hii wakili Yaasir Abdurahim alitoa shukrani kwa uongozi wa Ataba tukufu kutokana na msaada wao endelevu wa kuandaa semina kama hizi ambazo ni msaada mkubwa kwa mawakili, hakika semina hizi zinawasaidia kufikia ndoto zao na mwisho wa yote ni faida kwa jamii yetu na nchi yetu.

Fahamu kua semina ilihusisha mawakili wa kiume na kike takriban 25, ilifanyika katika ukumbi wa (Amid nadwaat wal mu-utamaraat) uliopo katika jengo la Kafeel la kitamaduni lililo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbaiyya tukufu
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: