Kumalizika kwa maonyesho ya vitabu vya watoto ya kimataifa katika mji wa Karbala na kamati ya maandalizi yawakirimu kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Ukumbi wa Khatamul Anbiyaa (s.a.w.w) katika Atabatu Husseiniya ulishuhudia hafla ya kuhitimisha maonyesho ya vitabu vya watoto ya pili kufanywa na Atabatu Husseiniyya tukufu kitengo cha malezi na makuzi ya watoto yaliyo fanyika kuanzia (15-24 Rabiul Awwal) na zilishiriki nchi nyingi na taasisi za uchapaji na usambazaji wa viyabu vya watoto.

Mkuu wa kitengo cha malezi na makuzi ya watoto cha Atabatu Husseiniyya tukufu Ustadhi Saadi Al banaau katika khutuba yake, aliwashukuru wote walio shiriki katika maonyesho haya ya kitamaduni na akawaomba waendelee kushiriki katika maonyesho kama haya kwa ajili ya kusaidia utamaduni wa watoto, alielezea pia mambo yaliyo onyeshwa na kitengo hicho, akasisitiza kua wataendelea na shughuli hizi kwa lengo la kutoa huduma bora zaidi kwa watoto wa nchi hii ambao ndio viongozi wa kesho.

Naye rais wa kitengo hicho ustadhi Muhammad Alhasanawiy alisema kua:

“Hakika maonyesho haya yalifanyika kwa mnasaba wa maulidi ya mtume mtukufu na yamehudhuriwa na nchi za kiarabu na za kieneo miongoni mwa nchi hizo ni: Lebanon, Saudia na Misri, pia vilishiriki vituo maarufu vya usambazaji wa vitabu vya watoto vinavyo zungumzia makuzi ya mwanadamu, na vitabu vya visa vya uhai wa watu wa nyumba ya mtume (s.a.w.w) vya lugha tofauti, hali kadhalika maonyesho haya yalikua na warsha kila siku, watumishi wa vituo vya usambazaji walikutana na kubadilishana uzoefu na kuhimizana kuhusu tamaduni za watoto”.

Akaashiria kua: “Warsha hizi zitazaa vipengele vitakavyo saidia katika kuboresha tabia za watoto kutakua na utafiti maalumu kuhusu swala hili”.

Fahamu kua maonyesho ya kimataifa ya vitabu vya watoto yaliyo fanyika hapa Karbala, ni maonyesho ya kwanza rasmi kufanyika hapa Iraq, na ni miongoni mwa moja ya harakati za kitengo cha ulezi na ukuzi wa watoto chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu, maonyeso haya yatafanywa kila mwaka na vitashiriki vituo vya usambazaji wa vitabu vya watoto vya ndani na nje ya Iraq, na huonyeshwa vitabu bora zaidi na machapisho ya mwisho katika uga wa watoto.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: