Kwa mara ya kwanza katika historia ya hauza zetu tukufu: Atabatu Abbasiyya tukufu katika mji wa Najafu yafungua hauza ya kimtandao kwa masomo ya moja kwa moja ..

Maoni katika picha
Hauza ya kwanza ya kimtandao katika historia ya mama wa hauza za kielimu (katika mji wa Najafu mtukufu) imeanzishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa jina la (Maahadi ya turathi za mitume kwa masomo ya hauza kwa njia ya mtandao), mkuu wa Maahadi hiyo, shekhe Hassan Turabi alisema kua:

“Sababu ya kufikiria kuanzishwa kwa mtandao huu ilitokana na wingi wa maombi tunayo pata katika mji wa Najafu kutoka nje ya nchi ya watu wanao taka kuja kusoma na hatuna uwezo wa kuwapokea hivyo tumeanzisha mtandao huu kama njia mbadala ya wao kuja”.

Akaendelea kusema kua: “Mbadala huu umekuja kwa kuzingatia mambo muhimu, maombi mengi yalitoka kwa wanawake walioingia madhehebu ya Ahlulbait (a.s) jambo ambalo ni vigumu kuwapokea hapa Najafu”.

Kuhusu utaratibu wa mtandao mpya shekhe Turabi alifafanua kua: “Maahadi ina utaratibu wa ndani, unaobainishwa katika mtandao rasmi, unamuwezesha kusoma mwanafunzi wa ndani na nje ya Iraq, hali kadhalika kuna masomo ya ndani ya Maahadi yenyewe kwa wanafunzi wanaopenda kuja kujiunga na masomo ya hauza, na kwa sasa tuna kiwango cha masomo ya awali (muqadimaat) na tuna walimu mahiri wa hauza”.

Akaendelea kusema kua: “Maahadi husambaza masomo ya hauza kwa njia ya teknolojia ya kisasa na masomo yanayo rushwa mtandaoni hua imma ni ya picha au maandishi na kuna uwezekano wa kujadiliana kati ya mwanafunzi na mwalimu kwa kila somo, Maahadi inawahakikishia wanafunzi wake njia bora ya kufanya mitihani kwa njia ya kimtandao, mwanafunzi kwa urahisi kabisa kutoka nchi yeyote ataweza kufanya mtihani wake aliyo tangaziwa na kwa muda wowote, pia ataweza kuangalia matokeo na max za mitihani yake, vile vile tunawawezesha wanafunzi kuwasiliana na walimu wao mojo kwa moja kwa kutumia simu za kisasa (smart phone) au kwa kutumia kompyuta (talakilishi) kwa kupitia intarnet”. Mkuu wa Maahadi alifafanua kuhusu majengo kua: “Kwa ajili ya uhusiano wa kiroho na hauza ya Najafu tukufu iliyo anzishwa zaidi ya miaka (1000) iliyo pita Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kiongozi wake wa kisheria Sayyid Ahmad Swafi (d.i) walichagua sehemu ya kujenga Maahadi iwe katika mji wa kale wa Najafu tukufu katika nyumba ya Allaama Sayyid Ridha Dini Almar ashiy, nyuma ya msikiti wa Shekhe Al answaariy.

Toghut ya Maahadi ya turathi za mitume ya masomo ya hauza ni:

http://www.turath-alanbiaa.org/index.php
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: