Warsha ya kielimu: kitengo cha uhandisi kimefanya warsha ya kielimu kujadili vikwazo vya kiutendaji

Maoni katika picha
Kitengo cha uhandisi katika Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na mkaguzi mkuu wa wakfu ya Shia wamefanya warsha katika ukumbi wa imam Qassim (a.s) uliopo ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kujadili mitihani ambayo hupuuzwa katika utendani.

Warsha hii ni miongoni mwa warsha na nadwa ambazo hufanywa na kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ilihudhuriwa na rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi Dhiyaau Swaaigh na msaidizi wa ofisi ya mkaguzi mkuu wa wakfu ya shia Ustadhi Muhammad Ally Daud na jopo la walimu, wahandisi na wanahabari, Dr. Hussam Ally Muhammad alizungumzia utambuzi wa matatizo na namna ya kuyatatua na kunufaika nayo na akatoa mifano halisi katika miradi inayo fanywa na Ataba tukufu.

Naye muhandisi Dhiyaau Swaaigh rais wa kitengo cha miradi katika Atabatu Abbasiyya alisema kua: “Leo kituo cha utafiti cha Alkafeel kilicho chini ya kitengo chetu kinafanya warsha ya kikazi kwa kushirikisha jopo la wahandisi kutoka katika Ataba na Mazaru mbalimbali kwa ajili ya kujadili mambo maalumu yanayo husu miradi ya Ataba na namna ya kuiendeleza kielimu kwa kutumia njia za kisasa au kutatua matatizo yanayo jitokeza, na leo tumejadili utambuzi wa matatizo yasiyo pewa umuhimu (madogi madogo)”.

Ustadhi Muhammad Ally Daud msaidizi wa mkaguzi mkuu wa wakfu ya Shia aliongeza kusema kua: “Warsha hizi zinaongeza kiwango cha ujuzi wa muhandisi na kumfanya aendelee kua mtafiti wa kisasa, hakika lengo la warsha hizi ni kuangalia namna ya kutatua matatizo wanayo kumbana nayo wahandisi katika utekelezaji wa miradi, na baadhi ya matatizo hayo yalikua yameorodheshwa na ofisi ya mkaguzi mkuu wa wakfu ya Shia”.

Warsha ilihudhuriwa na wahandisi (30) kutoka katika vitengo vya wahandisi wa Ataba mbalimbali na Mazaru matukufu na itadumu kwa siku mbili, pia ilipambwa kwa maswali na michango ya kielimu kutoka kwa washiriki jambo lililo onyesha ustadi wa washiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: