Mtiririko wa khutuba za Ijumaa waonyesha nuru

Maoni katika picha
Kituo cha (Ameed Duwalliy lilbuhuth wa Dirasaat) kitengo cha mtiririko (mausua) na vitabu kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa jarida la kumi na moja lenye juzuu mbili lililo kusanya (khutuba za Ijumaa za mwaka 2015 m/1436-1437 h) zilizo fanyiwa uhakiki wa kielimu na zaweza kua misingi ya marejeo kwa watafiti na wanafunzi wa masomo ya juu.

Dr. Karim Hussein Naaswih, rais wa kitengo cha mausua na vitabu amesema kua: “Hakika amefanya juhudi marjaa mkuu wa dini katika mji wa Najafu mtukufu katika kuelezea njia za tablighi na kufundisha maadili mema katika jamii ya kiislamu pamoja na kubainisha mambo yanayo faa jamii na namna ya kutatua matatizo yanayo jitokeza kwa kufata mafundisho ya mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) na maimamu watakasifu (a.s), khutuba za Ijumaa zinazo tolewa na wakili wa marjaa dini mkuu Sayyid Ally Sistani (d.dh) katika mji wa Karbala zimekua na umuhimu na athari kubwa katika jamii, kutokana na ujumbe zinao beba, ikiwa ni; mambo ya kifiqhi, kielimu, kitamaduni, kisiasa, kijamii na namna ya kutatua matatizo katika jamii kwa kuelekeza ufumbuzi wenye kufanikisha”.

Akaendelea kusema kua: “Hiyo imekua ni muhimu kuzihakiki khutuba hizi kwa kuangalia aya na haditi za mtume pamoja na maneno ya maimamu katika vitabu rejea na kurekebisha makossa ya kilugha na ki imla (kiuandishi)”.

Akaendelea kusema kua: “Hakika swala ya Ijumaa ina khutuba mbili, ya kwanza: huzungumzia utafiti wa kielimu uliochambuliwa kutoka katika vitabu tegemezi na hufafanuliwa mambo mbali mbali ya kisheria, ama khutuba ya pili: huzungumzia mambo ya kisiana, kiuchumii na huangalia matatizo yanayo ikumba jamii na namna ya kuyatatua na hutolewa nasaha zinazo kubalika katika vichwa vha wenye akili timamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: