Hospitali ya rufaa ya Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetuma jopo la madaktari walio bobea katika kutibu majeraha kwenda kuwatibu majeruhi wa Hashdi Shaabiy waliopata majeraha katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuihami Iraq na maeneo yake matukufu.
Kiongozi mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Alkafeel daktari Haidari Albahaadiliy alielezea kua: “Hakika uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu tangu wafungue Hospitali hii walijiwekea vipawa mbele vyao na miongoni mwa vipawa mbele hivyo ni kuwasaidia na kuwatibu wapiganaji watukufu ambao wamejitolea damu zao kwa ajili ya kubakiza heshima ya nchi yetu na kuzuia isinajisiwe na magaidi ya kidaishi, hivyo hupokea majeruhi kwa kuwasiliana na madaktari wa Hashdi Shaabiy au kwa mawasiliano ya moja kwa moja kupitia picha zilizo wekwa na Hospitali”.
Akaendelea kusema kua: “Kutokana na ufatiliaji wetu tuligundua kua; kuna haja ya kuagiza madaktari kutoka nje ya Iraq na ndio tukaagiza jopo la madaktari kutoka Iran walio bobea katika kutibu majeraha, wakiongozwa na Daktari Abulfadhil Baaqiriy, Hospitali iliandaa mazingira na vifaa kwa ajili ya kutoa huduma hii tukufu, madaktari hao walifanya uchambuzi na kutibu majeruhi (153) ikiwemo na kufanyiwa upasuaji kwa wajio hitajia, na miongovi mwa zana zilizo tumika ni kifaa cha (Ilizarov) ambacho ni kifaa nadra hapa Iraq”.
Akafafanua kua: “Hakika hii sio ziara ya kwanza kwetu, tumesha fanya ziara kama hizi siku za nyuma, tunayo yapata katika hospitali ya Alkafeel yanatufanya tuendelee kua na ziara kama hizi”.
Kumbuka kua Hospitali ya rufaa ya Alkafeel kutokana na maelekezo mfululizo inayo pata kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) inatoa umuhimu mkubwa kwa majeruhi wa jeshi la serikali na wale wa Hashdi Shaabiy na imesha pokea mamia ya majeruhi.