Kukamilika kwa mradi wa kwanza wa Alkafeel unao husu majengo ya makazi na kazi yaendelea katika sehemu za watumishi..

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, muhandisi Dhiyaau Majid Swaaigh ametangaza kukamilika kwa mradi wa nyumba za Alkafee za makazi zifikazo (831), kimsingi kazi ya ujenzi imekamilika sasa hivi kazi inaendelea katika sehemu za watumishi ambayo itaisha hivi karibuni.

Akaendelea kusema kua: “Hakika ujenzi wa nyumba hizi umefanywa kwa kufata ramani iliyo pangwa, kuanzia upembuzi wa majengo na vitu vitakavyo wekwa ndani yake, kitengo kilitoa kila aina ya msaada uliohitajika kwa watekelezaji wa mradi huu ilikuhakikisha unaisha kwa muda ulio pangwa”.

Naye kiongozi wa kambuni ya Almunqidhah (iliyo tekeleza mradi huu) ustadhi Maahir Abdul ameer Salmaan alisema kua: “Baada ya kumaliza ujenzi wa nyumba za makazi katika awamu zote (39) tumeanza kutengeneza maeneo ya watumishi, watakao ishi ndani ya majengo haya, na hii ilikua plani yetu kuanzia mwanzo, kuna sehemu ambazo zilijengwa sambamba na ujenzi wa nyumba na sehemu zingine tulisubiri hadi ujenzi wa nyumba ukamilike ndio tuzijenge”.

Akaendelea kusema kua: “miongoni mwa kazi zinazo endelea sasa hivi ni:

Kwanza: Utekelezaji na ufatiliaji pamoja na njia kuu na ndogo.

Pili: Shule, kuanzia: chekechea, msingi na upili (sekondari).

Tatu: sehemu ya kuogelea.

Nne: Kituo kikuu cha miradi.

Tano: Sehemu za biashara (maduka).

Sita: Benki ya taifa

Saba: Kituo cha watoto.

Nane: Ukumbi wa michezo.

Tisa: Kituo cha afya.

Kumi: Kuchonga barabara kuu na ndogo na kuziwekea alama.

Kumi na moja: Kuweka nyaya za umeme, baada ya kukamilika kwa uwekaji na nguzo hapo awali.

Asilimia kubwa ya kazi hizi tutatangaza ukamilifu wake, mradi huu umepambwa na nembo ya Atabatu Abbasiyya tukufu isipokua baadhi ya sehemu zenye harakati nyingi za mitambo”.

Ikumbukwe kua mkuu wa kambuni siku za nyuma aliahidi kua: “Atakamilisha na kukabidhi mradi kwa muda ulio pangwa, uchelewaji ulio tokea upo nje ya uwezo wetu, tunamshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu, pia kutokana na ushirikiano mkubwa tulio pata kutoka kwa Atabatu Abbasiyya tukufu tumeweza kuvuka vikwazo vyote tulivyo kutana navyo, na sisi kama kampuni tunafahamu wazi hali ya kiuchumi inayo ikumba Iraq kwa sasa na kadhalika inayo ikuta Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na hivyo hii haikua sababu ya kukwama kwa mradi wetu bali uliendelea kama ulivyo pangwa”.

Tunapenda ifahamike kua lengo la mradi huu ni kuonyesha thamani ya juhudi zinazo fanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuwahudumia watu wanaokuja kufanya ziara kwa Abulfadhili Abbasi (a.s) na kwa ajili ya kuwapatia makazi yanayo endana nao, watapewa nyumba hizi kwa bei ndogo yenye msaada ndani yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: