Umewasili ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu ukiongozwa na Shekh Amaar Alhilali rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika hafla ya kuhitimisha mashindano ya sita kitafa ya Qur an tukufu, upande wa usomaji na kuhifadhi, yaliyo andaliwa na uongozi wa Masjidi Kufa ukishirikiana na Mazaru zilizo chini yake.
Katika hafla hiyo yalitangazwa majina ya washindi wa usomaji na kuhifadhi, mashidano haya yalikua na washiriki (40) kutoka katika mikoa (18), iliundwa kamati ya majaji (10) wa kutoa hukumu katika mashindano haya.
Mashindano yalifanyika siku mbili mfululizo, katika hifhu na usomaji, na matokeo yalikua kama ifatavyo: upande wa hifdhu; mshindi wa kwanza alikua ni, Haafidh Maalik Abdulkaadhim kutoka katika mji wa Bagdad.
Mshindi wa pili alikua ni, Haafidh Hussein Khalil kutoka katika mkoa wa Samaawah.
Mshindi wa tatu alikua ni, Haafidh Muhammad Ridha Salmaan kutoka katika mkoa wa Kuut.
Upande wa usomaji; Mshindi wa kwanza alikua ni, Mujibu Mahmoud Daruwesh kutoka katika mkoa wa Diyala.
Mshindi wa pili alikua ni, Ridha Alaau kutoka katika mkoa wa Najafu.
Nafasi ya tatu waligongana wasomaji wawili ambao ni, Hussam Hameed kutoka Diwaniyyah na Aayadunillahu Wardiy kutoka Suleimaniyyah.
Shekh Ammaar Alhilali alisifu mashindano haya kua yanafaida kubwa na matokeo mazuri, sawa katika upande wa kuhifadhi au usomaji, na akatamani kuendelezwa harakati hizi za kufanya mashindano ya Qur an na kuyapanua zaidi kama sehemu ya kuutumikia uislamu na kueneza mafundisho yake kwa kupitia usomaji wa Qur an tukufu.
Tunapenda kukumbusha kua; Uongozi wa Masjid Kufa katika harakati hizi za Qur an tukufu unalenga kusambaza tabia njema zinazo endana na Qur an tukufu kwa vijana, na kupambana na fikra potofu zinazo shambulia umma wa kiislamu.