Atabatu Abbasiyya yapeleka shehena ya misaada kwa wapiganaji wa Hashdi Shaabiy katika mkoa wa Mosul..

Maoni katika picha
Bado Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kuwasiliana kwa karibu na wapiganaji shujaa tangu kutolewa kwa fatwa tukufu (ya jihadi ya kujilinda) hadi sasa, katika kutembelea vikosi mbali mbali vya wapiganaji wa Hashdi Shaabiy walio msitari wa mbele wa mapambano unao wazingira Daishi na kuzuia wasifikiwe na msaada wowote.

Ziara iliyo dumu kwa siku tano tuliwatembelea: kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, Saraya Jihadi na Kataibu Sayyid Shuhadaa na vinginevyo, katika miji ya; Tal abatwa, Tal zaltwa na Bartwala pamoja na miji mingine iliyo kombolewa hivi karikuni, kutokana na ushujaa wa wapiganaji wetu watukufu.

Rais wa ujumbe Shekh Haidari Al aaridhiy kutoka katika kitengo cha dini aliiambia Alkaafeel kua: “Kama mnavyo fahamu, Atabatu Abbasiyya tukufu tangu kutangazwa kwa fatwa na marjaa mkuu wa dini hadi leo tumekua msitari wa mbele kutembelea vikosi vya wapiganaji katika uwanja wa vita na kutoa misaada ya kimada na kimaanawi (hali na mali), na miongoni mwake ni huu msafara wa leo katika mkoa wa mosul, katika miji iliyo kombolewa na wanajeshi wa serikali pamoja na wale wa Hashdi Shaabiy.

Na shehena hii ni zawadi kutoka katika ofisi ya Marjaa dini mkuu Sayyid Ali Alhusseini Sistaani (d.dh.w) kwa maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i), tunatarajia kugawa vitu vya lazima kwa maelufu ya wapiganaji, kama vile; mablangenti, mavazi, mavazi ya nvua, soksi za mikono, kofia za baridi, na vinginevyo, hususan kutokana na hali ya baridi kali iliyopo katika mji wa Mosul hivi sasa”.

Akaendelea kusema kua: “Ziara iliyo dumu kwa siku tano, ilijumuisha vikosi mbali mbali vya wapiganaji, kama vile: (Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, Saraya Jihadi, Kataaibu Sayyd Shuhadaa (a.s), Liwaau Answaar Marjiiyyah, Kikosi cha Imam Ali (a.s) cha wapiganaji, Liwaau 30/ katika wapiganaji wa shabak) vikosi hivi vipo mstari wa mbele katika miji ya; Tal atwala, Tal zalatwa, Tal asira, Mahlabiyyah, na Bartwala katika ufukwe wa Nainawa. Kwa hakika katika kila ziara tunayo kuja kuwatembelea hawa wapiganaji tunawakuta katika ari ya juu kabisa, hii sio ajabu kwao kwani mtu anaye acha familia na mali zake na akaja hapa, bila shaka lazima awe na hamasa na moyo wa ushujaa wa kuhakikisha anawatoa maadui katika aridhi ya Iraq”.

Akaendelea kusema kua: “Sote tulikua tunafikiria namna gani wapiganaji wanaishi katika mazingira ya baridi kali sana wakiwa mbali na familia zao, lakini katika siku tulizo ishi nao tumegundua kua wanafarijika zaidi kwa kua kwao katika uwanja wa mapambano, na kumtoa adui kuliko kua pamoja na familia zao, huu ni ujumbe wa wazi kwa maadui waliokuja kuibomoa Iraq kua, wananchi wa Iraq wapo imara katika kulinda nchi yao na raia wake pamoja na maeneo matukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: