Pamoja na mazingira magumu ya hali ya hewa na kiusalama, kitengo cha misaada kilicho chini ya ofisi ya Marjaa dini mkuu Sayyid Ali Alhusseini Sistani (d.dh) kimeendelea kua pamoja na familia za wakimbizi wa Mosul au walio toka Huwaijah, waliokimbia mateso ya magaidi wa kidaish, misafara ya kutoa misaada inaendelea kama ilivyo pangwa, katika mahema ya wakimbizi na katika miji iliyo kombolewa, kitongo kimeongeza safari katika kipindi hiki kutokana na kuongezeka kwa wakimbizi na mahitaji, hivyo kitengo hiki kimekua pamoja nao kwa ajili ya kuwasidia kadri ya uwezo wake.
Radi amali (matokeo) ya misaada hiyo kutoka kwa familia zinazo pata misaada ni mmiminiko wa salamu na shukrani kwa Marjaa dini mkuu Sayyid Ali Alhusseini Sistani (d.dh), ambazo wamewabebesha kitengo cha misaada, miongoni mwa salamu hizo ni: ((Sayyid Sistani madamu hajatusahau na sisi katu hatuta msahau katika dua)).
Hayo yalisemwa na mkimbizi Hassan Shaami aliyopo karibu na mto wa khaazir sehemu ya Hassan Shaami ambayo ina familia za wakimbizi (2500) kutoka Mosul zenye watu elufu kumi, walipewa vikapu vya chakula (2500) na maziwa ya watoto pamoja na nguo za watoto za umri tofauti na nguo za wanawake (3500) na pakti za maji, walifurahi sana kwa misaada hiyo, na wakatoa shukrani kubwa kwa Marjaa dini mkuu.
Mwingine alisema kua: ((Tunamshukuru Sayyid Sistani kwa kutusimamia kama baba yetu na kusaidia katika mazingira magumu, hakika hatujawahi kupata msaada mkubwa wa kiasi hiki isipokua kutoka kwake yeye ambaye huruma yake ni kwa wairaqi wote bila kujali tabaka zao)). Haya yalisemwa na mkimbizi katika kambi ya Qimaawah katika mkoa wa Dahuuk ambapo kuna familia (1000) za wakimbizi kutoka katika miji ya Talkif na pembezoni mwake miongoni mwa vitongoji vya Nainawa, hawa tuliwapa vikapu (1000) vya chakula pamoja na nguo za watoto na maziwa ya watoto.
((Ujumbe wetu kwa Sayyid Sistani ni kwamba: mna malipo na thawabu , na Mwenyezi Mungu atakulipeni malipo bora zaidi enyi ndugu zetu na utukufu wetu, Mwenyezi Mungu awahifadhini, Allah Allah kwa kila familia inayo inua mikono yake juu na kukuomba wapatie taufiq na afya, ewe Mola wanusuru na uwahifadhi)). Haya yalisemwa na mkimbizi wa Huwaijah katika kijiji cha Rabidhwa na kijiji cha Samrah na baadhi ya wakimbizi wa Tikrit, walipewa vikapu (1500) vya chakula na mablangeti (22800) na maziwa ya watoto, misaada hii ilijumuisha pia wakimbizi wa Tal abatwa katika hema lililopo upande wa mji wa Qayarah lenye familia za wakimbizi elufu moja hawa tuliwapa shehena kubwa ya mavazi ya kujikinga na baridi.
((Aliye zima moto wa fitina hapa Iraq ni Sayyid Sistani hakika tumefahamu njama za maadui wa Iraq)).
Haya yalisemwa na wakimbizi wa miji ya kusini mwa Mosul nayo ni: Khaalidiyya, Ainu marmiyya, Khabaatwa, Makuuk, Sayyid Aawah, Swalaahiyya, Nasru, Ainu muzaan, Sultan Abdallah na Duwaizaat nao ni familia (3700) pamoja na wakimbizi waliopo katika hema la Qayarah familia (1300) kutoka katika mji wa Shura, walipewa vikapu elufu tano vya chakula.
((Tunamshukuru Sayyid Sistani, hakika hajatusahau, ameinua vichwa vyetu baada ya kudhalilishwa na daishi kwa fatwa yake tukufu ya kulinda nchi na maeneo matukufu)). Haya yalisemwa na wakimbizi wa vijiji vya Sab’awiin vilivyopo upande wa kulia wa mto Dujla kusini mwa mji wa Mosul ambao walipewa vikapu vya chakula elufu tatu na mia saba, kila familia kikapu kimoja chenye aina nane za vyakula, chakula hicho kiliwatosha watu (20,000) pia wakimbizi waliopo katika hema ya Jad’ah wapatao familia (1350) walipewa vikapu vya chakula kwa kila familia kikapu kimoja.
Hali kadhalika kwa wakimbizi wa hema la Hassan Shaami waliopo katika mji wa Hassan Shaami kutoka katika miji iliyo kombolewa huko Mosul ambayo ni: Kokujali, Bartwala, Baaziwaayya, na mtaa wa Karama na mitaa mingine nao walipewa vikapu elufu moja na mia moja hamsini kwa kila familia kikapu kimoja cha chakula.
Kumbuka kua kitengo cha misaada kinaendelea kutoa misaada mbali mbali kwa wakimbizi muda wote kwa ajili ya kupunguza machungu yao, na kuwafanya wahisi kua Marjaa mkuu ni kimbilio muhimu kwa wairaq wote bila kujali tabaka zao, na kuondoa sura mbaya inayo wekwa na maadui zetu.